Thursday, 20 July 2017

*MUHIMU KWA WALIOMALIZA DIPLOMA NA KIDATO CHA SITA ILI KUFANYA UDAHILI KUINGIA CHUO KIKUU*

1.Kwa waliomaliza Cheti na Diploma wanatakiwa kuwasilisha nyaraka zao NACTE ili zihakikiwe(verification) kupitia Link ambayo imetolewa kupitia mtandao wa *NACTE* baada ya uhakiki huo utapewa *code namba* kulingana na ufaulu wako ambayo ndio itakuwezesha kufanya *UDAHILI* kwenye chuo kikuu unachokipenda,kumbuka Hakuna chuo kitapokea maombi ya udahili bila code namba hiyo,zoezi limeshaanza na linaendelea Hadi sasa .

2.Kwa walimaliza Kidato cha Sita maombi UDAHILI kwa mwaka huu Unafanyika moja Kwa moja  kupitia chuo na sio *TCU* kama miaka iliyopita, UDAHILI utaanza *tarehe 22.07.2017* hadi *30.08.2017*,hivyo mwanafunzi atafanya maombi ya kusoma shahada kupitia chuo anachokipenda, vyuo vikuu vyote vimeshapewa maelekezo kupitia maafisa UDAHILI (admission officers) kupitia mafunzo maalum yaliyoisha tarehe 15.07.2017,Kitu cha muhimu ni kwamba mwanafunzi hatolazimika kusafiri kwenda chuo husika kila kitu kitafanyika kupitia mtandaoni (Online), Anachotakiwa kufanya mwanafunzi ataingia kwenye *Website* ya chuo utatafuta *link* ya udahili na kufata taratibu ambazo zimeweka.

Mwanafunzi atajaza taarifa chache Sana ,maana chuo kinamuingilano Wa *mfumo data* na NECTA na NACTE, mwanafunzi atajaza taarifa muhimu tu ikiwa ni Pamoja na majina, index namba zote Hata kama uliwahi ku Reseat zaidi ya mara moja,email na code namba kwa waliomaliza Cheti na Diploma.

Muda uliotengwa ukiisha baada ya tarehe *30.08.2017* hakutakuwa na nyongeza ya muda .

Baada ya hapo majina yatatolewa kwa kila chuo na mwanafunzi aliyedahiliwa atathibitisha usomaji wake kwenye chuo kimoja hata kama jina lake limejitokeza kwa vyuo zaidi ya kimoja.

NB: Maelekezo zaidi yanapatikana kupitia

*www.nacte.go.tz kisha Bofya Award verification*

*www.tcu.go.tz kisha Bofya Admission procedures for 2017/18*  uzisome kwa umakini na kuzielewa kuepuka kusumbuka dirisha likifunguliwa

No comments:

Post a Comment

Comments system

KATEMBO JR BLOG

J.P. KATEMBO

JACKSON PHOCUS KATEMBO