1.HAKIKISHA UNA AKIBA NZURI YA PESA KABLA HUJATOA TAARIFA RASMI ZA KWENDA UKWENI!
Unapotaka kwenda ukweni kwa mara ya kwanza (kupeleka mahari au posa na mahari kwa wakati mmoja) unatakiwa kujiandaa kifedha kwa sababu wewe (mwanaume )ndio mhusika mkuu. Kuna gharama hujitokeza kama vile usafiri, posho ya mshenga, posho ya wazee wako wanaokusindikiza, chakula njiani, kununua vitu vinavyoambatana na mahari nakadhalika. Hata kama ndugu zako watakuchangia kwa upendo lakini ujue kitendo cha wewe kushindwa kufanya maandalizi hayo kitatafsiri kwamba hujajiandaa kuoa kwa hiyo unaweza kuwakatisha tamaa ndugu na jamaa zako wa karibu. Ndugu hujisikia amani wanapoona unamudu gharama za hapa na pale na utaona jinsi watakavyojitokea zaidi hadi wakati wa harusi.
2.USIWAOGOPE WAKWE ZAKO!
Sehemu ya ugenini hususan kwa wakwe kwa kweli sio sehemu inayozoeleka kiuwepesi lakini ukifahamu kwamba hao ni ndugu zako itakusaidia kupunguza hofu. Hata hivyo unapaswa kuwa na ujasiri kwa sababu kama mtarajiwa wako amekubali wewe na ndugu zako kufika kwao maana yake umepata kibali kwao kwa sababu wazazi wanafurahi wanapoona vijana wanaoana kwa kufuata utaratibu mzuri badala ya kuchukuana na kuanza kuishi kimya kimya. Kama umegundua wazazi wa mtarajiwa wako hawakukubali labda kwa sababu ya kipato chako kidogo, au labda wana mtu mwingine ambaye walimchagulia binti yao akamkataa usioneshe kuwachukia hata kidogo bali jifanye huelewi kinachoendelea, onesha kuwafurahia na kuwaheshimu ili umalize kazi yako uchukue mke uondoke. Kumbuka ndoa ni kati yako na mtoto wao, japokuwa tunahitaji baraka za wazazi lakini haina maana watuchagulie wenza wa maisha kwa hiyo kama binti yao anakukubali na ana amani kuishi na wewe usijali kadiri siku zinavyoenda wakwe zako watakupenda hadi utashangaa.
3.IJUE SAIKOLOJIA YA MASHEMEJI.
Mashemeji wanaweza kukufanya urudi tena au usitamani kurudi tena ukweni. Mashemeji ni watu wa kwanza kukujadili kwa hiyo jipange kwa hilo. Ni vizuri kabla ya kwenda ukweni uwe na urafiki na mashemeji (hata kama sio wote) ili kupunguza hali ya kujiona mgeni ukweni. Ukishindwa kuwa rafiki na mashemeji na kujua maendeleo yao na ikiwezekana kuwasaidia kwenye mahitaji madogo madogo (kabla na baada ya kuoa dada yao) unatengeneza hali ya kutothaminiwa au kudharauliwa na wakati mwingine wanaweza wasikufurahia wakidhani unamtesa dada yao (kwa ubahili au umaskini wako). Kwa hiyo unapoonana na mashemeji ongea nao, furahi nao na ikiwezekana nenda nao matembezini ili wakuone kama sehemu ya familia yao, hapo watakupa heshima na upendo ule ule wanaompa dada yao(mke w
No comments:
Post a Comment