HISTORIA YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliundwa mnamo tarehe 26 Aprili,
1964 kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (inayojumuisha
Visiwa vya Pemba na Unguja). Tanganyika ilikuwa ni mwendelezo wa
koloni la Ujerumani, utawala wa Waingereza kwa Mamlaka ya Umoja
wa Mataifa, Himaya ya Umoja wa Mataifa chini ya utawala wa
Uingereza na mwisho Taifa huru kuanzia mwaka 1961 ndani ya nchi
za Jumuiya ya Madola.
Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ziliingia
mkataba wa Muungano mnamo mwaka 1964 na kuanzishwa Dola ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mkataba huu wa Muungano
ulitiwa saini na aliyekuwa Rais wa Tanganyika, Hayati Mwalimu
Julius Nyerere na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid
Amani Karume tarehe 22 Aprili 1964 huko Zanzibar. Mkataba huo
ulithibitishwa na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi hapo
tarehe 26 Aprili, 1964 na mnamo tarehe 27 Aprili, 1964, viongozi wa
nchi zote mbili walikutana katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es
Salaam na kubadilishana Hati za Muungano. Sheria za Muungano
zilitoa tamko la Jamhuri ya Muungano katika Ibara ya 4 kwamba:
“Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zitalazimika,
baada ya kuungana na siku zote baada ya kuungana, kuunganishwa
kuwa Dola ya Jamhuri kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika
na Zanzibar’ (Ibara ya 4 Sheria za Muungano)

Jina hili la “Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar”
lilibadilishwa baadae mnamo tarehe 28 Oktoba, 1964 na kuwa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia Sheria ya Jamhuri ya
Muungano, Sheria namba 61 ya mwaka 1964.
Watanganyika kama ilivyokuwa kwa wananchi wa nchi nyingine za
kiafrika, hawakukubaliana hata kidogo na utawala wa kikoloni. Tangu
mwanzo waliwapinga na kupigana na wavamizi wa kikoloni, upinzani
mkubwa ukionyeshwa na Wasambaa wakiongozwa na Kimweri dhidi
ya Wajerumani, Wahehe wakiongozwa na Mkwawa kupigana
vichungu na virefu dhidi ya Wajerumani na wakati wa vita vya Maji
Maji chini ya uongozi wa Kinjekitile, Mputa na Kibasila.
Kukosekana kwa umoja kati ya wapigania uhuru hawa wa mwanzo
na uimara wa majeshi ya wakoloni na silaha bora za moto
kulidhoofisha mapambano haya ya uhuru na kusababisha hasara
kubwa na kupoteza maisha ya watu.
Kama ilivyokuwa kwenye makoloni mengi ya Kiafrika, hisia za Utaifa
ziliendelea kuimarika katika Tanganyika baada ya mwaka 1945.
Alama za utaifa zilishaanza kuonekana punde baada ya vita kuu ya
kwanza ya dunia kwa kuanzishwa kwa vyama mbalimbali vya
Waafrika kwa upande wa Tanganyika na Zanzibar. Kwa upande wa
Tanganyika, African Association ilianzishwa mwaka 1929 kama
kikundi cha mijadala baina ya wasomi na ilipofika mwaka 1948 chama hiki kikawa Tanganyika African Association (TAA). Baada ya Vita ya Pili ya Dunia, wanachama wa Tanganyika African Association(TAA) waliendeleza wimbi la utaifa. Mwaka 1953 chini ya uongozi waMwalimu Nyerere, TAA ilitambuliwa kama chama cha siasa na
kuelekea moja kwa moja kuanzishwa kwa TANU mwaka 1954iliyotumika kama chombo cha kisiasa cha watu katika kutoa vilio vyaovya kudai uhuru. Kuanzishwa kwa TANU mwaka 1954, ulikuwa ndio
mwanzo wa mbio za kupigania uhuru. Baada ya miaka saba yamapambano ya kisiasa, Tanganyika ilikuwa huru chini ya chama chaTANU,kilichoimarishwa na vyama vya wafanyakazi na vya ushirika.
Kwa upande wa Zanzibar, chimbuko la Jumuiya ya Waafrika ilikuwani vilabu vya mpira wa miguu vilivyoanzishwa mwanzoni mwa miakaya 1930. Ilipofika mwaka 1934, Jumuiya ya Waafrika ilianzishwarasmi na kupewa jina la African Association (AA). Baada ya vita ya
pili ya dunia kama ilivyokuwa katika sehemu nyingine za dunia,kulikumbwa na uhaba mkubwa wa chakula, ubaguzi na mgawanyiko
baina ya jamii. Kutokana na matatizo hayo ya ubaguzi, kulianzishwa
Jumuiya ya Washirazi (Shirazi Association) katika Visiwa vya Unguja
na Pemba lengo likiwa ni kudai kupatiwa haki mbalimbali za kijamii
na kulinda utambulisho wao. Kuundwa kwa chama cha ZNP
(Zanzibar Nationalist Party) mwaka 1957, kulifanya viongozi wa
Jumuiya ya Waafrika (African Association) na wale wa Shirazi
Association waone umuhimu wa kushirikiana. Waligundua kuwa
Serikali ya kikoloni na chama cha ZNP walishirikiana kuendeleza
dhuluma dhidi ya Waafrika. Viongozi hao waliona ulazima wa
kuungana kuwa kitu kimoja kupigania uhuru. Hivyo, katika kutekeleza
azma hiyo, Viongozi wa Jumuiya hizo walikutana na kukubaliana
kuunganisha Shirazi Association na African Association mwaka 1957
na kuunda chama kilichoitwa Afro- Shirazi Union ambacho baadae
kiliitwa Afro-Shirazi Party chini ya uongozi wa Sheikh Abeid Amani
Karume. Mwalimu Nyerere alishiriki katika mkutano huu. Ilikuwa
tarehe 05 Desemba, 1957 hapo mtaa wa Mwembekisonge Unguja.
Kati ya mwaka 1957 mara tu baada ya uchaguzi mkuu wa kwanza na
mwishoni mwa mwaka 1963, kabla ya mapinduzi ya mwaka 1964,
Zanzibar ilitawaliwa na vuguvugu na mivutano mikali ya kisiasa.
Mapambano haya ya kisiasa yalikuwa kati ya Chama cha Afro-Shirazi
kilichoungwa mkono na Waafrika na kile cha Zanzibar Nationalist
Party kilichoungwa mkono na Wakoloni, Sultani pamoja na jamii ya
Waarabu. Chama cha ZNP baada ya kushindwa uchaguzi, kilianzisha
kampeni za kushawishi wenye mashamba na mabepari wengine
wenye kumiliki njia kuu za uchumi, kuwafukuza kazi au kutowaajiri
wafuasi wa ASP. Halikadhalika, Chama cha ZNP kiliwatafutia kazi na
kuwabakisha mashambani Waafrika wote waliokubali kukiunga
mkono. Wakati wa mvutano huo wa kisiasa kati ya ASP na ZNP
ikipamba moto, kulijitokeza tofauti miongoni mwa viongozi wa ASP.
Tofauti hizo zilichangiwa na uroho wa madaraka, ubinafsi na
kutokuwa na msimamo imara miongoni mwa baadhi ya viongozi wa
chama hicho. Halikadhalika Serikali ya Sultani nayo ilichochea
migogoro hiyo ili ijinufaishe kisiasa. Migogoro hiyo ilipelekea kujitoa
kwa baadhi ya Viongozi wa ASP ambao walifanya mkutano na
baadhi ya wanasiasa mashuhuri wa ASP huko Pemba Novemba,
1959 na kukubaliana kuanzisha Chama kipya cha siasa cha Zanzibar
and Pemba People’s Party (ZPPP) na Sheikh Muhammed Shamte
kuwa Mwenyekiti. Wakati vyama vya ASP, ZNP na ZPPP vikiwa
katika malumbano makali ya kisiasa, Serikali ya Kikoloni ilifanya matayarisho ya uchaguzi wa pili. Uchaguzi ulifanyika tarehe 16
Januari, 1961 na siku moja kabla ya uchaguzi huo Serikali ilitangaza
kuwa chama kitakachoshinda kitaunda Serikali na Wizara zote
zitakuwa chini yake. Katika uchaguzi huo ASP ilishinda kwa kupata
viti 10, ZNP kilipata viti 9 na chama cha ZPPP kilipata viti 3. Kutokana
na kuenea kwa chuki za kisiasa miongoni mwa Wazanzibari, Vyama
vikuu vya kisiasa vilifikia muafaka wa kumaliza hali hiyo. Hatahivyo,
ASP haikufikisha zaidi ya nusu ya kura na hivyo haikuweza kuunda
Serikali. Hivyo njia pekee iliyobakia ilikuwa ni kuishauri ZPPP
ichanganye viti vyake na chama kimoja kati ya ASP na ZNP. ZPPP
na ZNP viliungana. Hatahivyo, iliamuliwa kuwa iundwe Serikali ya
muda na kusubiri uchaguzi mwingine uliopangwa kufanyika mwezi
Juni, 1961. Waingereza walitoa uhuru kwa Serikali ya Mseto ya ZNP/
ZPPP ya Waziri Mkuu Muhammed Shamte. Chini ya ushauri wa
Waingereza, Shamte aliwatenga ndani ya Serikali yake baadhi ya
viongozi wa ZNP wenye msimamo wa Kikomunisti wakiongozwa na
Abdulrahaman Babu, na hivyo kutokea kutofautiana kwa baadhi ya
viongozi wa ZNP na Serikali ya ZNP/ZPPP. Baada ya kutengwa na
Serikali hiyo walijitoa ZNP na kuanzisha Chama cha Umma. Chama
hicho kilivunjwa mara tu baada ya Mapinduzi ya mwaka 1964 na
hapo viongozi na wafuasi wake walijiunga na Serikali ya ASP chini ya
uongozi wa Abeid Karume.
Zanzibar ilikuwa na wakati mgumu katika kupigania uhuru.
Waingereza walijikita zaidi kwa madhumuni ya kibiashara na kwa nia
ya kukomesha biashara ya utumwa. Hii ilikuwa ni kwasababu,
walitaka nguvukazi rahisi ambayo ilikuwa inapotea kwa kufanywa watumwa kwa uzalishaji wa malighafi kwa ajili ya viwanda vyao
Ulaya, halikadhalika kutokana na Mapinduzi ya Viwanda Ulaya
yalisababisha Waingereza kuja kutafuta soko kwa ajili ya bidhaa zao.
Waingereza walifikia makubaliano na Sultani mwaka 1822 ili
kukomesha biashara ya utumwa, lakini ilichukua zaidi ya miaka 50
hadi utumwa kutokomezwa. Makubaliano ya Waingereza na
Wajerumani ya mwaka 1890 yalifanya Zanzibar kuwa koloni la
Waingereza ambao walimshirikisha Sultani katika utawala wao.
Waingereza waliainzisha ubaguzi wa rangi Zanzibar kwa Wazungu
na Waarabu kupendelewa kuwa tabaka la juu na Waafrika la chini.
Waingereza walifanya Zanzibar kuwa ni koloni la Waarabu na
ilipofika Desemba 1963, Sultani alipewa mamlaka kamili ya kutawala
Zanzibar. Tarehe 12 Januari 1964, aliyekuwa Sultani wa Zanzibar,
Jamshid bin Abdulla, aling’olewa madarakani katika Mapinduzi
yaliyokuwa yameandaliwa kwa usiri, ustadi na ujasiri mkubwa wa
Wanamapinduzi wa Afro-Shirazi Party (ASP) na Jamhuri
ikatangazwa.
Muundo wa Muungano wa Tanzania kama ulivyoelezwa katika Katiba
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, una vyombo viwili vyenye
mamlaka ya utendaji ambavyo ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano
na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Vyombo viwili vyenye mamlaka
ya kutekeleza utoaji haki ambavyo ni Mahakama ya Jamhuri ya
Muungano na Mahakama ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; na
vyombo viwili vyenye mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia
utekelezaji wa shughuli za umma ambavyo ni Bunge na Baraza la
Wawakilishi. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inashughulikia mambo yote ya Muungano kama yalivyoainishwa
katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977
na yasiyo ya Muungano kwa upande wa Tanzania Bara na Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar inayoshughulikia mambo yote yasiyo ya
Muungano kwa upande wa Tanzania Zanzibar.
Muungano wa Tanzania ni tukio la nadharia iliyotafsiriwa katika
vitendo, kwani kuunganisha Tanganyika na Zanzibar ilikuwa ni hatua
ya watu walio wakweli. Ni ushahidi unaojitosheleza kuwa wananchi
wa Tanganyika na wa Zanzibar wakiongozwa na viongozi wao wa
mapambano ya kudai uhuru, walitoa kauli zilizokuwa zikimaanisha
walichofikiri na kuazimia na wala siyo kwa sababu ya kusombwa na
jazba za kisiasa.

SABABU ZA KUWEPO KWA MUUNGANO
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umekuwepo kutokana na
sababu zifuatazo:-
sababu zifuatazo:-
1. Kuwepo kwa mahusiano ya karibu kihistoria baina ya
Tanganyika na Zanzibar katika nyanja mbalimbali kama vile
udugu wa damu, biashara, utamaduni, lugha na mahusiano ya
karibu kisiasa hususan baina ya TANU na ASP.

2. Moyo wa kuwa na Muungano wa Afrika hususan kwa kuanzia
na Shirikisho la Afrika Mashariki. Hata kabla ya uhuru wa
Tanganyika, Mwalimu Nyerere pamoja na viongozi wengine waliokuwa wakipigania utaifa katika ukanda wa Afrika Mashariki
walikuwa na matarajio ya kuwa na Muungano wa Afrika.
Mwalimu Nyerere binafsi alipendelea uwepo Muungano wa
Afrika kwa kuanzia na Mashirikisho ya kikanda. Baada ya
kushauriana na viongozi mbalimbali wa iliyokuwa Jumuiya ya
Wapigania Uhuru wa Afrika Mashariki na Kati (Pan- African
Freedom Movement for East and Central Africa - PAFMECA)
Mwalimu Nyerere alitoa tamko wakati wa mkutano wa nchi huru
za Afrika uliofanyika Addis Ababa mwaka 1960 kwamba;
“Wengi wetu tunakubaliana bila kikwazo kwamba Shirikisho laAfrika Mashariki litakuwa ni jambo zuri. Tumesema na ni kwelikwamba mipaka inayotenganisha nchi zetu imewekwa namabeberu na sio sisi wenyewe na kwamba tusikubali itumike dhidiya umoja wetu…lazima tuzisumbue ofisi za wakoloni kwa nia si ya
kudai uhuru wa Tanganyika, kisha Kenya, na Uganda halafuZanzibar lakini kwa nia ya kutaka uhuru wa Afrika Mashariki kamaMuungano mmoja wa Kisiasa”.(imeripotiwa kwenye gazeti laTanganyika Standard, Novemba 1964)Mapinduzi ya Zanzibar mnamo mwezi Januari, 1964 yalifanyikawakati Mwalimu Nyerere akiwa ameshachoshwa na kukatishwa
tamaa na mazungumzo ya Shirikisho la Afrika Mashariki.Mapinduzi haya yaliiweka madarakani Serikali ya chama chaASP kilichokuwa na mahusiano ya karibu na TANU kwaupande wa Tanganyika. Kwa uhakika zaidi, upo mchanganyiko wa sababu mbalimbali
za Muungano huu kama vile historia za nchi hizi mbili, ukaribu wa nchi hizi mbili, muingiliano wa kijamii, ushirikiano wa
kibiashara, ushirikiano madhubuti na wa muda mrefu wa kisiasa
baina ya TANU na ASP, ushirikiano na urafiki wa muda mrefu
kati ya watu, viongozi, na wakati wa harakati za utaifa
uliopelekea uhuru wa nchi hizo mbili, sababu za kiusalama n.k.

HATI YA MAKUBALIANO YA MUUNGANO
Msingi wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka
1977 na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ni Hati za Muungano za
mwaka 1964. Hati za Muungano zilitiwa saini na waasisi wa
Muungano tarehe 22 Aprili, 1964, na hapo Tanganyika na Zanzibar
kuwa dola moja, ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar. Mapatano ya Muungano yaliunganisha mataifa mawili
yaani Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar na
kuweka Taifa moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar kwa misingi ya Katiba na misingi inayotambulika Kimataifa.
Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
lilibadilishwa baadae na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Baada ya Muungano, Mwalimu J. K. Nyerere alikuwa Rais wa
kwanza na Sheikh Abeid Amani Karume, alikuwa Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tarehe 26 Aprili, 1964 Bunge la Tanganyika lilipitisha Sheria za
Muungano. Halikadhalika Sheria hizi zilithibitishwa na Baraza la
Mapinduzi Zanzibar. Sheria hizi za Muungano zilithibitisha Hati za
Muungano, zilitaja Rais na Makamu wa Rais, zilitaja Muundo wa
Muungano na Katiba ya Muungano. Mnamo tarehe 27 Aprili 1964 waasisi wa Muungano walibadilishana Hati za Muungano na
wajumbe saba (7) wa Baraza la Mapinduzi waliapishwa kuwa
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar ambao ni: Sheikh Abeid Amani Karume, Bw. Kassim Abdala
Hanga, Bw. Abdulrahaman Mohamed Babu, Sheikh Hassan Nassor
Moyo, Sheikh Aboud Jumbe, Sheikh Hasnu Makame na Sheikh Idris
Abdul Wakil. Wote hawa walifanya Mawaziri wa Serikali ya
Muungano. Kati ya Viongozi hawa wawili wako hai hadi sasa. Nao ni
Aboud Jumbe na Hassan Nassor Moyo.
Kabla ya siku ya Muungano, kulikuwa na Katiba mbili; Katiba ya
Tanganyika ya mwaka 1962 na upande wa Zanzibar kulikuwa na
Amri za Katiba (Constitution decrees). Katiba ya Tanganyika baada
ya kufanyiwa marekebisho iliendelea kutumika kama Katiba ya
Muungano wakati ule wa mpito, kuanzia tulipoungana hadi
ilipopitishwa Katiba ya Muungano kwa mujibu wa Makubaliano ya
Muungano na Sheria za Muungano. Aidha, marekebisho hayo
yalimtaja Rais wa Zanzibar kuwa ni Makamu wa kwanza wa Rais,
akiwa ni msaidizi wa Rais kwa masuala yote ya kiutawala kwa
upande wa Zanzibar, na Waziri Mkuu kuwa ni Makamu wa Pili wa
Rais ambaye atamsaidia Rais kwa masuala yahusuyo upande wa
Tanganyika na kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni.
Katiba ya muda ya mwaka 1965 ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania iliainisha mambo kumi na moja (11) ambayo yalikubalika
kuwa ni ya Muungano chini ya usimamizi wa Serikali ya Muungano.
Mambo hayo ni:-

• Katiba na Serikali ya Muungano
• Mambo ya Nchi za Nje
• Ulinzi
• Polisi
• Mamlaka juu ya mambo yanohusika na hali ya hatari
• Uraia
• Uhamiaji
• Mikopo na Biashara ya Nchi za Nje
• Utumishi katka Serikali ya Jamhuri ya Muungano
• Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika,
ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa
nchini Tanzania unaosimamiwa na Idara ya Forodha.
• Bandari mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na
simu.
Katiba ya muda ya mwaka 1965 ilianiainisha utawala wa Serikali ya
mfumo wa chama kimoja, TANU kwa Bara na ASP kwa Zanzibar.
Katiba hii, ilizingatia misingi ya Makubaliano ya Muungano ya mwaka
1964 na Sheria za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Katiba ya
muda ya mwaka 1965 iliainisha Serikali mbili, Uwakilishi wa Zanzibar
katika Bunge la Muungano na uongozi wa Serikali ya Zanzibar.
Serikali ya Muungano ikiwa na mamlaka juu ya mambo yote ya
Muungano na mambo yote yasiyo ya Muungano kwa upande wa
Tanganyika. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiwa na mamlaka juu
ya mambo yote yasiyo ya Muungano yahusuyo Zanzibar.

KUONGEZEKA KWA MAMBO YA MUUNGANO
Mambo ya Muungano yaliongezeka kutoka kumi na moja (11) hadi
ishirini na mbili (22) kutokana na mahitaji ya ndani ya wananchi
yaliyolenga kuunganika kwa mambo mengi zaidi pamoja na
mabadiliko yaliyokuwa yanaendelea kutokea ulimwenguni baada ya
Muungano.
Mwaka 1965, jambo la kumi na mbili linalohusu Mambo yote
yanayohusika na sarafu na fedha kwa ajili ya malipo yoyote halali
(pamoja na noti); mabenki (pamoja na mabenki ya kuweka akiba) na
shughuli zote za mabenki; fedha za kigeni na usimamizi juu ya
mambo yanayohusika na fedha za kigeni liliongezeka chini ya Katiba
ya muda ya mwaka 1965. Sababu kubwa ilikuwa ni kuwa na sarafu
ya pamoja ya Tanzania baada ya Muungano, na kurahisisha
usimamizi wa fedha za kigeni na mabenki katika Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Aidha, kufuatia kuundwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka
1967, mambo matatu ya Muungano yaliongezwa, ambayo ni; Leseni
za viwanda na takwimu; elimu ya juu; na usafiri na usafirishaji wa
anga.
Mwaka 1968, mambo ya maliasili ya mafuta, pamoja na mafuta
yasiyochujwa ya motokaa na ama ya petrol na aina nyinginezo za
mafuta au bidhaa na gesi asilia yaliongezwa kwenye orodha ya
mambo ya Muungano.
Aidha mambo ya Muungano yaliendelea kuongezeka hadi kufikia 21
kufuatia kuvunjika kwa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka
1977. Mambo yote yaliyokuwa ya upande wa Tanganyika na
Zanzibar yaliyokuwa yakisimamiwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki,
yalikabidhiwa kwa Serikali ya Muungano.
Mwaka 1992 kufuatia mabadiliko ya mfumo wa siasa nchini suala la
ishirini na mbili la uandikishaji wa vyama vya siasa na mambo
mengine yanayohusiana navyo liliongezwa kwenye orodha ya
mambo ya Muungano.
No comments:
Post a Comment